NAIBU KATIBU MKUU AFANYA ZIARA OFISI ZA SIDO MANYARA
Ili kufahamu zaidi huduma za SIDO kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, Naibu Waziri Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Hashil T. Abdallah amefanya ziara katika ofisi ya SIDO mkoa wa Manyara. Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa ni kujifunza na kujua namna Ofisi za SIDO kanda zinavyosaidia SMEs kupitia huduma zake mbalimbali zinazotolewa.