Katalogi ya Mafunzo

Catalogi ya Mafunzo imesheheni mkusanyiko wa mafunzo mbalimbali na Maelezo ya mafunzo hayo kwa kina, unapohitaji kupata taarifa zaidi kuhusiana na aina Fulani ya mafunzo catalogi hii ya mafunzo inakupatia maelezo ya kina juu ya mafunzo hayo kuanzia ujumbe uliomo ndani ya mafunzo hayo, njia zitakazotumika katika kutoa mafunzo hayo, wateja waliolengwa na mafunzo hayo, gharama ya mafunzo hayo na muda ambao yatafanyika (siku,wiki au mwezi).

Malengo:
Mwisho wa program hii wahusika watakuwa na uwezo wa kuelewa namna ya kutengeneza na kuzalisha bidhaa za ngozi, uchaguzi wa vifaa na tabia za ngozi . Pia watakuwa na uwezo wa kutengeneza na kuzalisha bidhaa mbalimbali za ngozi kutoka kwenye ngozi zilizochakatwa na wao wenyewe.
Moduli:
 • Jina la moduli: 
  Bidhaa za ngozi na Uzalishaji wake
  Maelezo ya Moduli: 
  1.Maana ya ngozi (Ngozi mbaya na ngozi yenye ubora) 2.Uchaguzi wa vifaa . 3.Aina za mashine zinazotumika kwenye uchakataji wa ngozi . 4.zana na vifaa rahisi. 5.Uendeshaji wa cherehani. 6.Kutengeneza mikanda rahisi. 7.Kutengeneza folder za A4. 8.Kutengeneza mikoba ya kiofisi. 9.Utengenezaji wa waleti. 10. Utengenezaji wa mikoba ya shule. 11. Utengenezaji wa sendozi. 12. Utengenezaji wa viatu. 13. Kutengeneza vishikizo vya funguo za gari na makava ya simu.
Mbinu za kufundishia:
Kujifunza kwa kushirikishana/mafunzo hayo yanaweza kufanyika kwa kiswahili au kiingereza,kazi za makundi,Uwasilishaji,kazi binafsi nk.
Watu waliojifunza masuala ya uchakataji wa ngozi, watengeneza viatu na watu wanaojihusisha na ngozi.
Ada:
TZS 300,000/= kwa muhusika (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki tatu
Malengo:
Mwisho wa program hii wahusika watakuwa na ujuzi wa teknolojia kuhusu uzalishaji wa chaki na kuanzisha biashara za chaki.
Moduli:
 • Jina la moduli: 
  Teknolojia ya kutengeneza chaki
  Maelezo ya Moduli: 
  1.Kanuni ya uzalishaji chaki. 2.Uzalishaji wa chaki kwa vitendo. 3.Elimu kuhusu ujasiriamali. 4.Masoko. 5.Gharama. 6. Hatua za ufungaji wa bidhaa.
Mbinu za kufundishia:
Kujifunza kwa kushirikishana, Majadiliano kwa makundi, Uwasilishaji kwa kufundisha, kazi binafsi.
Viwanda vidogo vinavyotaka kuwekeza kwenye uzalishaji wa chaki.
Ada:
TZs150,000 kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki moja
Malengo:
Mwisho wa mfunzo haya wahusika watakuwa na uwezo wa kutengeneza vyerehani vyao.
Moduli:
 • Jina la moduli: 
  Kurekebisha na kutengeneza vyerehani.
  Maelezo ya Moduli: 
  . Jinsi ya kuchunguza vyerehani. 2.Kulitambua tatizo na kurekebisha. 3.Utunzaji na uendeshaji wa vyerehani. 4. . 5. Utunzaji wa vifaa. 6.Jinsi gani ya kuanzisha karakana ndogo ya kutengeneza na kurekebisha vyerehani.
Mbinu za kufundishia:
Kujifunza kwa kushirikiana,mafunzo kwa uwasilishaji,kujaribisha ujuzi uliopo/uliopatikan.
Vijana wadogo wenye dhamira ya kutumia vyerehani na kutaka kuanzisha karakana ndogo zinazohusiana na vyerehani.
Ada:
TZs 200,000 kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki nne
Malengo:
Mafundi vyerehani wadogo watakuwa na uwezo wa kubuni nguo za aina mbalimbali.
Moduli:
 • Jina la moduli: 
  Ubunifu wa Magauni.
  Maelezo ya Moduli: 
  1.Ujuzi wa kubuni nguo za aina mbalimbali. 2.Kuongeza ufundi katika shughuli ya ushonaji. 3.Kuongeza ujuzi kwenye mbinu za ukataji kitambaa na ushonaji wa nguo husika. 4.kuchunguza ubora wa gauni au nguo ya aina yoyote iliyoshonwa.
Mbinu za kufundishia:
Kujifunza kwa njia ya kushirikiana, majadiliano ya makundi, mazoezi.
Mafundi vyerehani wadogo.
Ada:
TZs150,000 kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki moja
Malengo:
Mwisho wa program hii mafundi cherehani watakuwa na ujuzi wa kutosha juu ya masuala ya kudarizi vitambaa.
Moduli:
 • Jina la moduli: 
  Utengenezaji wa darizi
  Maelezo ya Moduli: 
  1.Aina mbalimbali za darizi. 2.Ubunifu wa aina tofauti kwenye mashuka na foronya za mito 3.Ubunifu wa darizi za mashati na magauni. 4.Ubunifu wa darizi kwenye kushen za viti.
Mbinu za kufundishia:
Mafunzo kwa njia ya kushirikishana,mafunzo ya makundi,mafunzo kwa vitendo.
Mafundi vyerehani wadogo.
Ada:
TZs. 100,000 kwa muhusika mmoja (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki moja
Malengo:
Mwisho wa program hii , wahusika watakuwa na uwezo wa kuanzisha biashara,kubaki kwenye biashara zao na kuinua biashara zao.
Moduli:
 • Jina la moduli: 
  Moduli 1) Kujitambua
  Maelezo ya Moduli: 
  1. Tabia binafsi za mjasiriamali. 2. Kujitambua katika tabia za ujasiriamali. 3. Uzalishaji wa mawazo ya biashara. 4. Uchambuzi wa ndani na nje wa mawazo ya biashara.
 • Jina la moduli: 
  Moduli 2) Kuanzisha biashara yako.
  Maelezo ya Moduli: 
  1. Tabia binafsi za mjasiriamali. 2. Kujitambua katika tabia za ujasiriamali. 3. Uzalishaji wa mawazo ya biashara. 4. Uchambuzi wa ndani na nje wa mawazo ya biashara. 5. Uandaaji wa mpango wa biashara.
Mbinu za kufundishia:
Utumiaji wa njia za CEFE kama ushirikishwaji, Kujifunza kwa uzoefu, mazoezi, majadiliano ya makundi, uwasilishaji wa mtu binafsi.
Wanaoanza, Waliopo pamoja na viwanda vya kati na vidogo.
Ada:
250,000/T.sh kwa muhusika (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki mbili
Malengo:
Uchakataji wa ngozi na rasilimali zilizopo.
Moduli:
 • Jina la moduli: 
  Teknolojia ya uchakataji wa ngozi
  Maelezo ya Moduli: 
  1.Maana ya uchakataji wa ngozi. 2.Maelezo juu ya aina za ngozi. 3. Vyanzo vya ngozi na matumizi ya ngozi. 4.Matunzo mazuri ya ngozi toka mnyama akiwa hai mpaka anapochinjwa na ngozi kuchunwa. 5. Njia za utunzaji. 6. Sehemu ya kutunzia. 7. Matabaka ya ngozi. 8. Uandaaji wa vifaa vya kufanyia kazi. 9. Uandaaji wa kileo kinachotumika kuchakatia ngozi. 10. Njia mbalimbali zinazotumika wakati wa uchakataji wa ngozi. 11. Kupima mafanikio baada ya kuchakata. 12. Ufafanuzi wa sehemu ya kuchakatia ngozi. 13. Kufahamu matatizo. 14. Masuala ya mazingira..
Mbinu za kufundishia:
Mchanganyiko wa mafunzo kwa njia ya ushirikishaji, majadiliano ya makundi na mafunzo kwa vitendo.
Washikadau wa ngozi,wajasiriamali walio tayari kuanzisha viwanda katika sekta ya ngozi pamoja na wajasiriamali ambao tayari wanazalisha bidhaa zitokanazo na ngozi.
Ada:
TZS 300,000/= kwa muhusika (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki tatu
Malengo:
Ni kubadilisha pamba iwe kwenye nguo yenye urembo na nguo yenye kukubalika katika soko na ushindani, kuhamisha ujuzi na ufundi wa kutengeneza batiki na kuwawezesha wahusika/wateja kuanzisha biashara/ viwanda vyao.
Moduli:
 • Jina la moduli: 
  Utengenezaji wa Batiki
  Maelezo ya Moduli: 
  1.Maana ya utengenezaji wa Batiki. 2.Mafunzo kuhusu utengenezaji wa Batiki. 3.Aina na njia mbalimbali za utengenezaji wa Batiki. 4.Mafunzo ya vitendo katika utengenezaji wa Batiki. 5.Ubunifu wa Batiki. 6.Ramani ya kiwanda na usalama.
Mbinu za kufundishia:
Utumiaji wa njia ya ushirikishaji,mafunzo kwa nadharia,utumiaji wa michezo na mafunzo ya kutembelea sehemu ambayo Batiki inatengenezwa.
Wanaoanza biashara na waliopo tayari kwenye biashara.
Ada:
TZS 300,000/= kwa muhusika (ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki tatu
Malengo:
Kuwawezesha wahusika/wateja kupata ujuzi /mbinu za kutengeneza sabuni za vipande na sabuni za maji, kuwawezesha wateja kuanzisha viwanda vyao wenyewe / Biashara na kuwawezesha wateja kuzalisha sabuni zenye masoko na ushindani.
Moduli:
 • Jina la moduli: 
  Utengenezaji wa Sabuni
  Maelezo ya Moduli: 
  1.Maana ya sabuni. 2.Vitu vitumikavyo kutengeneza sabuni. 3.Aina ya utengenezaji wa sabuni. 4.Hatua za uzalishaji. 5.Gharama ya uzalishaji sabuni na bei ya sabuni. 6.Sabuni maalum. 7.Ramani ya kiwanda na usafiri.
Mbinu za kufundishia:
Mafunzo kwa nadharia,Mafunzo kwa vitendo, Michezo,Chemshabongo,kujifunza kwa kutembelea na stori za ushuhuda.
Wanaotaka kuanza na waliopo tayari kwenye uzalishaji
Ada:
TZs 250,000 kwa muhusika mmoja(ada,chakula na steshonari)
Muda:
wiki moja.
Malengo:
Kuwawezesha wasindikaji kujua jeli (Watermelon Jelly) ya tikitimaji inavyosindikwa.
Moduli:
 • Jina la moduli: 
  Usindikaji wa jeli ya tikitimaji
  Maelezo ya Moduli: 
  Maelezo ya moduli: - 1. Usafi na Usalama wa jeli ya tikitimaji 2. Vifaa vitakiwavyo katika usindikaji wa jeli ya tikitimaji. 3. Mafunzo ya nadharia na vitendo. 4. Ufungashaji wa jeli ya tikitimaji. 5. Mahesabu ya gharama na upangaji wa bei.
Mbinu za kufundishia:
Mbinu za kufundishia ni: - 1. Njia ya mafunzo kwa ushirikishwaji. 2. Kujifunza kwa vitendo.
Wasindikaji wapya na waliopo kwenye sekta kwa muda mrefu..
Ada:
Shilingi za Kitanzania 100,000/= kwa kila mshiriki. Hii ni gharama ya ada na steshonari. Bidhaa mbili zitafundishwa za aina tofauti.
Muda:
Wiki moja.

Jeli ya tikitimaji inasindikwa kutokana na juisi ya tikitimaji. Mahitaji mengine yanayohitajika katika usindikaji wa jeli ya tikiti maji ni: -

1. Juisi ya tikitimaji.

2. Sukari.

3. Tangawizi mbichi.

4. Pectin.

5. Citric acid.

 

Usindikaji wa jeli ya tikitimaji hauna tofauti na usindikaji wa aina nyingine za jamu. Tofauti iliyopo ni mahitaji yanayotakiwa katika utengenezaji wa jamu hizo.

Pages