Mradi wa Kuendeleza Ujasiriamali Vijijini (MUVI)

SIDO iko katika utekelezaji wa mradi kwa kutoa huduma kwa miradi ya wajasiriamali vijijini chini ya dhana ya Mlolongo wa thamani ili kuongeza kipato chao na kupunguza umasikini. 
 
Mradi unafadhiliwa na IFAD, SIDO inatekeleza uendeshaji wa mradi chini ya Wizara ya Viwand ana Biashara na unatekelezwa katika mikoa na mazao yaliyoteuliwa kama ifuatayo; Ruvuma (Muhogo,Mahindi na Alizeti), Iringa (Nyanya, Serena na Alizeti), Pwani (Muhogo, Ufuta na Matunda), Tanga (Matunda, Maharagwe na Alizeti), Manyara (Mifugo na Alizeti) na Mwanza (Muhogo, Mpunga na Alizeti). Utekelezaji halisi wa shughuli za mradi unafanywa na wataalamu waelekezi waliopewa mikataba ya kazi, na utekelezaji unaendelea. 
 
Wananchi washiriki wamefundishwa mbinu bora za kilimo, biashara, kuwezeshwa kuanzisha miradi ya uongezaji thamani mazao yao na kupata masoko ya uhakika ya mazao yao na bidhaa zake.