Mradi wa kuwawezesha Wanawake Katika Kilimo (Kuwaki)

Swahili
Katika mwaka 2014, SIDO Singida ikishirikiana na Helvetas Swiss Interco operation and Community Development and Relief Trust (CODERT) waliandaa mpango kuimarisha wakulima wadogo wa mboga mboga katika uzalishaji na masoko.Mradi unafadhiriwa na Umoja wa Ulaya.
 
Utekelezaji unafanywa na mashirika matatu ambayo ni Helvetas, SIDO and CODERT wakishirikiana na Halmashauri za Wilaya za Singida Vijijini , Mkalama na Iramba mkoani Singida, HOT Tengeru, ASA, Mradi wa Maji kwa ajili ya Dunia ya Tatu (Water for third world (W3W), AVRDC na Wizara ya kilim.
 
Utelezaji wa mradi unawashirikisha wazalishaji 100 na umelenga kuongeza na kuboresha uzalishaji, maendeleo na biashara katika mwelekeo wa maendeleo ya kiuchumi na kupunguza umasikini katika mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla kwa kuimarisha mnyororo wa thamani na kuwaunganisha wazalishaji wadogo wa mboga na masoko.