Programu za Mikopo

SIDO ina mifuko miwili  ya  utoaji wa Mikopo. Mfuko wa Taifa wa Kuendeleza Wajasiriamali  (NEDF) na Mfuko wa Mzunguko wa Mkoa (RRF) kwa mtu mmoja mmoja na kwa vikundi.

MFUKO WA TAIFA WA WAFANYABIASHARA WANANCHI (NEDF)
VIELELEZO VYA MKOPO

Kiasi: Shilingi 500,000- 5,000,000 za kitanzania
Muda wa marejesho: Mpaka Miaka 3 kulingana na aina na ukubwa wa mradi.
kiwango cha riba: 18% kwa mwaka kwa sekta ya uzalishaji (redusing balance)
Riba ni 22% kwa mwaka kwa sekta zisizo za uzalishaji (reducing balance)
Malipo ya huduma: 2% ya kiasi cha mkopo

MASHARITI /TARATIBU ZA UTOAJI WA MKOPO
a) Muombaji awe mkazi na raia wa Tanzania
b) Mradi/Biashara unaoombewa mkopo uwe umesajiliwa kihalali na wenye uwezo wa kukopesheka.
c) Makazi ya muombaji yawe ya kudumu na yanatambulika na kiongozi wa Serikali za Mtaa.
d) Muombaji wa mkopo awe ndie mmliki halali wa mkopo/biashara.
e) Muombaji awe na uwezo na nia ya kurejesha mkopo kwa muda uliopangwa.
f)Muombaji wa Mkopo awe tayari kufungua Akaunti ya Benki kwa jina la biashara yake.
g) Kwenye  mikopo ya mtu mmoja mmoja muombaji awe na wadhamini wawili wenye dhamana zinazozidi asilimia 125 ya thamani ya mkopo.
h) Kwenye mikopo ya vikundi muombaji awe tayari kujiunga kwenye vikundi vya mashikamano na kuweka akiba ya mkopo kama dhamana ya mkopo.

WALENGWA
Wafanyabiashara wanaoanza na wenye biashara zilizopo.

MFUKO WA MZUNGUKO WA MIKOANI (RRF)
VIELELEZO VYA MKOPO
Kiasi: TZS.500,000- TZS.6,500,000
Kipindi cha malipo: Mpaka Miaka 3 kulingana na aina ya mradi
Awamu za ulipaji: kila mwezi
kiwango cha riba: 22% kwa mwaka kwa ajili ya uzalishaji na sekta isiyo uzalishaji (reducing balance)
malipo ya huduma : 2% ya kiasi cha mkopo.

MASHARTI/TARATIBU ZA UTOAJI MIKOPO
Mikopo hutolewa kwenye Ofisi za SIDO zilizoko kwenye mikoa yote ya Tanzania bara  baada ya muombaji kukidhi  mashariti na vigezo vifuatavyo:-
a) Muombaji awe mkazi na raia wa Tanzania
b) Mradi/Biashara unaombewa mkopo uwe umesajiliwa kihalali na wenye uwezo wa kukopesheka.
c) Makazi ya muombaji yawe ya kudumu na yanatambulika na kiongozi wa Serikali za Mtaa.
d) Muombaji wa mkopo awe ndie mmliki halali wa mkopo/biashara
e) Muombaji awe na uwezo na nia ya kurejesha mkopo kwa muda uliopangwa.
f)Muombaji wa Mkopo awe tayari kufungua Akaunti ya Benki kwa jina la biashara yake.
g) Kwenye  mikopo ya mtu mmoja mmoja muombaji awe na wadhamini wawili wenye dhamana zinazozidi asilimia 125 ya thamani ya mkopo.
h) Kwenye mikopo ya vikundi muombaji awe tayari kujiunga kwenye vikundi vya mashikamano na kuweka akiba ya mkopo kama dhamana ya mkopo.

WALENGWA
Wafanyabiashara wanaoanza na wenye biashara zilizopo.
MIKOPO YA VIKUNDI
VIELELEZO YA MKOPO

Kiasi cha mkopo: Shilingi 100,000 Shilingi 500,000
muda wa marejesho: miezi 6 hadi mwaka 1 (kwa wiki au kwa mwezi)
Kiasi cha riba: 18% kwa mwaka
Malipo ya Huduma: 2% ya kiasi cha mkopo mkopo
Akiba: 20% ya kiasi cha mkopo

MASHARITI /MAHITAJI NA TARATIBU ZA UTOAJI WA MKOPO