Upatikanaji wa mitaji kwa Wajasiriamali wadogo na wakati ni moja kati ya changamoto zinazowakabili Wajasiriamali wengi nchini. Wajasiriamali wadogo na wakati hawana uwezo wa kukopa kwa kukosa dhamana zinazokubalika na taasisi za kifedha (regulated FIs).
Sababu hizi ndizo zilizopelekea Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kuanzia mpango wa udhamini kwa wajasiriamali wadogo kupitia ruzuku iliyotolewa na Mfuko wa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Japan.
Lengo la mpango huu ni kuwasaidia Wajasiriamali wadogo na wakati kwenye kukuza uchumi kwa kuwajengea mazingira mazuri ili waweze kukopeshwa na benki kwa unafuu wa dhamana.
Walengwa wa Programu hii ni wajasiriamali wadogo na wakati wenye miradi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara waliofuzu kupitia mikopo mingine inayotolewa na SIDO kama mfuko wa taifa wa kuendeleza Wajasiriamli wadogo (NEDF)
MPANGO WA DHAMANA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO
Huu ni mpango mpya unaosimamiwa na kutekelezwa kwa pamoja baina ya SIDO na Benki ya CRDB kwenye mikoa saba ambayo ni;Morogoro,Dodoma,Singida,Manyara,Arusha,Kilimanjaro na Mbeya.
Mpango huu unakusudia Benki ya CRDB PLC kutoa mikopo kwa Wajasiriamali wadogo na wakati walioko kwenye miradi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na Kilimo Biashara walioidhinishwa na SIDO.
VIELELEZO VYA MPANGO WA DHAMANA
Miradi inayohusika na Mpango: Uzalishaji wa mazao ya kilimo na Kilimo Biashara
Riba ya Mkopo: 20% Pamoja na kipindi cha msamaha (grace period)
Mikoa inayotekeleza:Mikoa saba (7) ya Morogoro,Dodoma,Singida,Manayara,Arusha,Kilimanjaro na Mbeya.
Kiwango cha Mkopo: Kuazia Tshs.5000, 000/= hado Shs.50, 000,000/=
Muda wa Marejesho: Kuanzia miezi sita (6) hadi miezi thelathini na sita (36)
Ada ya huduma: 1% (inayolipwa SIDO)
Mpango wa dhamana unatekelezwa na SIDO na Benki ya CRDB kwa kuzingatia mashariti yafuatayo:-
1. Wajasiriamali wenye miradi ya uzalishaji ya sekta ya kilimo na Kilimo Biashara
2. Wajasimali walengwa waliofuzu kwenye mikopo inayotolewa na SIDO kupitia mfuko wa kuendeleza wajasiriamali wadogo (NEDF