UGAWAJI WA VITENDEA KAZI KWA MAFUNDI WADOGO - KIABAKARI

SIDO Mara kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali toka Nchini Wales liitwalo TFSR CYMRU (Tools For Self Reliance) wametoa vifaa mbalimbali kwa mafundi wadogo wenye viwanda vidogo vya Useremala, Ushonaji, Uhunzi, Mechanics, Baiskeli na Viatu. Mradi huu ulianzishwa kwa lengo la kupunguza uhaba wa vitendea kazi kwa mafundi wadogo hasa maeneo ya vijijini ambayo yameonekana kuwa na changamoto nyingi katika upatikanaji wa vitendea kazi. Kwa Mkoa wa Mara mradi umegawa vitendea kazi kwa wilaya za Musoma mjini, Musoma Vijijini, Butiama, Rorya, Serengeti, Tarime na Bunda. Mafundi ambao wamefanikiwa kupata vitendea kazi katika Wilaya hizi wamekuwa wakifanya kazi kwa urahisi na ufanisi, pia ubora katika vitu wanavyozalisha umeendelea kuimalika kutokana kuwa na vitendea kazi vizuri. TFSR CYMRU baada ya kutembelea Wilaya ya Butiama na kuona wingi wa Mafundi katika Kata ya Kukirango wanaofanya kazi zinazofanana kama vile Ushonaji, useremala, Uhunzi na Ufundi wa kutengeneza Baiskeli waliamua kusaidia upatikanaji wa vitendea kazi kwa mafundi hao kwa mfumo wa Kongano ( CLUSTER) kwa maana ya mafundi wanaofanya kazi zinazofanana kupatiwa vifaa ili waweze kutumia kwa pamoja kwa vile ambavyo ni haviwezi kugawiwa kwa kila kikundi kuwekwa katika kituo kimoja ambacho mafundi watafika na kufanya kazi zao kwa urahisi. Kwa Kipindi cha Mwaka mmoja na nusu vikundi 127 vimeweza kupatiwa vitendea kazi ikiwa ni 58 kwa wanawake washonaji na 69 kwa wanaume katika nyanja za useremali, Uhunzi, Ufundi Baiskeli, Utengenezaji wa Viatu na Mechanics (ufundi wa kutengeneza pikipiki).

Swahili
Main Image: